Ikiwa unatokea kwenye asili ya ukimbizi au mtafuta hifadhi unaweza kustahiki Chekechea ya Kuanza Mapema (ESK). ESK inaweza kusaidia kuhakikisha kuwa unapata kiwango cha juu zaidi cha saa za mpango wa Chekechea ya Watoto Bila Malipo kila wiki kwa ajili ya mtoto wako.
Jinsi ya kuomba
ESK inapatikana katika programu zote za chekechea zinazotolewa na mwalimu aliyehitimu. Unaweza kumwandikisha mtoto wako kwa kuwasiliana na chekechea iliyo karibu nawe na kuomba kupata ruzuku ya Chekechea ya Kuanza Mapema. Huduma za Chekechea zinaweza kufikia huduma ya utafsiri bila malipo ili kukusaidia katika lugha yako.
Unaweza pia kuwasiliana na Idara ya Elimu ya Shule ya Chekechea ya Miaka Mitatu kupitia Simu ya Maulizo kwa 1800 338 663 au baraza lako la mtaa kwa usaidizi. Ili kupata usaidizi katika lugha yako unaweza kupiga simu kwa Huduma ya Kitaifa ya Utafsiri na Ukalimani kwa nambari 131 450, omba mkalimani apige simu nambari ya halmashauri ya eneo lako au Idara ya Elimu, na mkalimani atakaa kwenye simu na kutafsiri.
Wakati wa kuomba
Watoto wanastahiki ESK iwapo watafikisha miaka mitatu kabla ya tarehe 30 Aprili mwaka ambao wamejiandikisha kuhudhuria Shule ya Chekechea ya Miaka Mitatu. Tazama ‘ni lini kujiandikisha’.
Ikiwa mtoto wako amezaliwa kati ya tarehe 1 Januari na 30 Aprili unaweza kuchagua mwaka gani ataanza Shule ya Chekechea ya Miaka Mitatu. Mtoto wako anaweza kuanza Chekechea ya Umri wa Miaka Mitatu katika mwaka huo huo anapofikisha miaka 3, au mwaka anapofikisha miaka 4. Ikiwa mtoto wako anaanza Shule ya Chekechea ya Miaka Mitatu katika mwaka anapofikisha miaka 3 basi ataanza shule mwaka anapofikisha miaka 5. Ikiwa unachagua kumpeleka mtoto wako katika Shule ya Chekechea ya Miaka Mitatu katika mwaka atakapofikisha miaka 4, ataanza shule mwaka atakapofikisha miaka 6.
Iwapo unahitaji usaidizi kuhusu wakati mtoto wako anastahiki ESK, unaweza kuwasiliana na Idara ya Elimu, halmashauri ya eneo lako, muuguzi wako wa afya ya uzazi na mtoto, au chekechea katika eneo lako, au mojawapo ya mashirika yafuatayo katika eneo lako.
- Laini ya kuuliza maswala ya Chekechea kwa Miaka Mitatu 1800 338 663
- Brotherhood of St Laurence 03 9483 1183
- Foundation House 03 9389 8900
- Huduma za Watoto za Fka 03 9428 4471
- VICSEG New Futures 03 9383 2533
Je, mtoto wangu anapaswa kwenda kwenye Chekechea ya Umri wa Miaka Minne?
Ndiyo, watoto ambao wamefikia Shule ya Chekechea ya Awali pia wanastahiki Chekechea ya Watoto wa Miaka Minne bila malipo au ya gharama nafuu. Shule ya Chekechea ya Umri wa Miaka Minne inakua polepole kuwa Maandalizi ya Mapema, kuanzia 2025. Mnamo 2026, hadi saa 25 za Maandalizi ya Mapema zitapatikana kila wiki kwa watoto ambao:
- wanatoka katika mazingira ya mkimbizi au mtafuta hifadhi
- wanaojitambua kama Waaboriginal na/au Torres Strait Islander
- ambaye familia yake imewahi kuwa na mwingiliano na ulinzi wa mtoto (child protection)
Kujiandikisha kupitia ESK katika mwaka uliopita huhakikisha kwamba mtoto wako anaweza kufikia saa za Maandalizi ya Mapema zilizoongezwa kila wiki bila kujali anapoishi wapi Victoria. Familia zitastahiki Maandalizi ya Mapema hata kama hazijajiandikisha katika ESK katika mwaka uliopita.
Updated